• Home
  • About
  • ProjectsVisit here to see our organizational projects
  • News and Blog
  • Contact Us

TASA Yashiriki Kuchimba Msingi wa Kituo cha Afya Nalingu Katika Jitihada Za Kudumisha Amani na Maendeleo

February 23, 2026

Tasa Tanzania

Uncategorized

Timu ya TASA ikiwa pamoja na Wananchi wa Kata ya nalingu katika shughuli ya kijamii ya kuchimba msingi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Nalingu. Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya kuimarisha huduma za kijamii huku ikichochea umoja na mshikamano miongoni mwa wakazi wa eneo hilo.

Katika tukio hilo la kihistoria, TASA iliungana na Wanamabadiliko wa kata hiyo kupitia mradi wa Amani Yetu Kesho Yetu. Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhili wa shirika la CEFA Tanzania kupitia programu ya Kujenga Amani Project inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union in Tanzania).

Ushiriki huu ulikuwa na lengo kuu la kuonyesha mshikamano na umoja wa vijana na wanawake katika kudumisha amani. TASA inaamini kuwa amani ya kweli inajengwa kupitia kazi za pamoja zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja na kuchochea maendeleo ya jamii kwa haraka.

Kitendo cha kuchimba msingi wa kituo hiki cha afya ni kielelezo tosha kuwa amani na maendeleo ni vitu vinavyotegemeana. Kupitia nguvu za pamoja kati ya TASA, Wanamabadiliko, na wananchi wa Nalingu, jamii inaonyesha utayari wa kulinda amani ya kesho kwa kujenga miundombinu muhimu leo.

Tukio hili limeacha alama ya ushirikiano mkubwa na ni mwendelezo wa jitihada za TASA katika kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele kwenye harakati za amani na maendeleo nchini Tanzania.

Previous: TASA Yaimarisha Uandishi wa Maandiko Miradi na Usimamizi wa Ruzuku, Ikiwa ni Sehemu ya Pili Ya Utekelezaji wa OCD chini ya Vijana Plus Project
Next: TASA Yaangazia Umuhimu Wa majukwaa Ya Kidigitali Katika Kupanua wigo Kiutendaji Kwa Upande wa NGOs Tanzania.

Search

Archives

  • March 2026
  • February 2026
  • October 2025

Categories

  • Uncategorized

About TASA

TASA is a Non Governmental Organization committed to fostering safety society, free from violence. Guided by its vision of a safe and inclusive environment, the Alliance promotes safety standards through public education, stakeholder engagement, and advocacy for policy and legal reforms.

Quick Links

  • Home
  • About
  • ProjectsVisit here to see our organizational projects
  • News and Blog
  • Contact Us

Contact Info

Physical Address: Mtwara-Tanzania Mtwara MC, chuno street (Map is attached in About Us Page)

Phone: +255786388501
E-mail: [email protected]
Website: https://tanzaniasafetyalliance.org

© Copyright 2026 Tanzania Safety Alliance. All Rights Reserved

English
Swahili