• Home
  • About
  • ProjectsVisit here to see our organizational projects
  • News and Blog
  • Contact Us

Viongozi wa Serikali na Dini Nanguruwe Wapokea kwa Kishindo Program ya VIJANA@rtWORK kutoka TASA

March 2, 2026

Tasa Tanzania

Uncategorized

Tanzania Safety Alliance (TASA) imepiga hatua nyingine muhimu katika kuwafikia vijana kwa kufanya mkutano wa utambulisho wa mradi (Inception Meeting) katika Kata ya Nanguruwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini. Mkutano huu ulihusisha wadau wa serikali na viongozi wa dini kwa lengo la kuelezea dhima ya mradi na kuimarisha ushirikiano wa ngazi ya msingi.

Sanaa na Uhifadhi wa Mazingira

Kama NGO Mtwara inayojidhatiti katika mabadiliko ya kijamii, TASA inatekeleza mradi wa VIJANA@rtWORK unaolenga kutumia nguvu ya sanaa na ubunifu kama daraja la kuhamasisha vijana katika utunzaji wa mazingira. Mradi huu pia unasisitiza usawa wa kijinsia katika kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, ukiamini kuwa sanaa ni nyenzo thabiti ya kuleta uelewa na ushiriki wa jamii.

Mapokezi ya Wadau na Viongozi

Viongozi wa serikali na dini katika kata ya Nanguruwe wameupokea mradi huu kwa muitikio mkubwa na kuahidi ushirikiano wa dhati. TASA inaamini kuwa kupitia viongozi hawa, elimu ya utunzaji wa mazingira itawafikia vijana wengi na kuleta matokeo chanya katika uhifadhi wa asili.

Ushirikiano wa Kimkakati

Mradi wa VIJANA@rtWORK unafadhiliwa na CDEA kupitia @goethetanzania na Umoja wa Ulaya (@euintanzania). Huu ni muendelezo wa jitihada za TASA kuhakikisha vijana wanakuwa mstari wa mbele katika kutumia vipaji vyao kwa ajili ya maendeleo endelevu na utunzaji wa mazingira nchini.

Previous: TASA Yaangazia Umuhimu Wa majukwaa Ya Kidigitali Katika Kupanua wigo Kiutendaji Kwa Upande wa NGOs Tanzania.
Next: TASA Yatambulisha Mradi wa Kuwawezesha Vijana na wanawake kuwa Wastahimilivu Kwa Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usawa wa Kijinsia Wilayani Newala

Search

Archives

  • March 2026
  • February 2026
  • October 2025

Categories

  • Uncategorized

About TASA

TASA is a Non Governmental Organization committed to fostering safety society, free from violence. Guided by its vision of a safe and inclusive environment, the Alliance promotes safety standards through public education, stakeholder engagement, and advocacy for policy and legal reforms.

Quick Links

  • Home
  • About
  • ProjectsVisit here to see our organizational projects
  • News and Blog
  • Contact Us

Contact Info

Physical Address: Mtwara-Tanzania Mtwara MC, chuno street (Map is attached in About Us Page)

Phone: +255786388501
E-mail: [email protected]
Website: https://tanzaniasafetyalliance.org

© Copyright 2026 Tanzania Safety Alliance. All Rights Reserved

English
Swahili