TASA Yatambulisha Mradi wa Kuwawezesha Vijana na wanawake kuwa Wastahimilivu Kwa Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usawa wa Kijinsia Wilayani Newala
NEWALA, MTWARA – Katika muendelezo wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Tanzania Safety Alliance (TASA) imefanya mkutano wa utambulisho (Inception Meeting) na wadau wa serikali pamoja na viongozi wa dini katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Mkutano huu umelenga kutambulisha rasmi mradi wa “Kuwawezesha Vijana na Wanawake kuwa Wastahimilivu dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi


