We Don’t Just Talk Safety, We Build It: Explore Our Range of Life-Changing Initiatives, Including

Miradi ya Kujenga Amani

TUDUMISHE AMANI KUPITIA ELIMU

Mradi huu ulitekelezwa chini ya Search for Common Ground kupitia mradi wa 'Kwa Pamoja Tudumishe Amani'. Mradi huu ulifanyika Mkoa wa Mtwara, ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (Mtwara DC), katika kata mbili za Madimba na Ziwani mnamo 2024.

Miradi ya Kujenga Amani

AMANI YETU MAENDELEO YETU

Mradi huu ulitekelezwa mwaka 2025 kwa kushirikiana na Search for Common Ground, katika Kata ya Msangamkuu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (Mtwara DC). Mradi huu ulikuwa ni mpango wa kujenga amani na uwezeshaji uliolenga kushughulikia unyanyapaa na dhana hasi (stereotypes) wanazokumbana nazo waendesha bodaboda ndani ya jamii.

Soma Zaidi
Miradi ya Amani na Usalama

SAUTI MOJA AMANI YETU

Mradi huu ulibuniwa ili kukuza majadiliano ya wazi na ya kujenga kati ya makundi mbalimbali ya jamii, wakati huo huo ukiimarisha ushirikiano kati ya jeshi la polisi, viongozi wa serikali za mitaa, na wanajamii.

Soma Zaidi
Miradi ya Haki na Usalama

AMANI YETU KESHO YETU

Mradi huu unalenga kushughulikia masuala yanayohusiana na Ukatili wa Kijinsia (GBV), ujenzi wa amani, na kuzuia utoro wa wanafunzi shuleni. Unatekelezwa kupitia klabu za ujenzi wa amani shuleni na Mabalozi wa Amani waliofunzwa, ambao wanahimiza majadiliano, uvumilivu, na maelewano ya pande zote miongoni mwa wanafunzi na wanajamii.

Soma Zaidi
Miradi ya Haki Za binadam

HEDHI SALAMA

Lengo la mradi huu ni kukuza afya na usafi wa hedhi miongoni mwa wasichana wadogo kwa kutoa upatikanaji wa taulo za hedhi salama, za bei nafuu, na zinazoweza kutumika tena, pamoja na elimu kuhusu usimamizi wa usafi wa hedhi. Mradi unalenga kushughulikia changamoto ambazo wasichana hukumbana nazo wakati wa hedhi, kama vile utoro wa shule, unyanyapaa, na ukosefu wa vifaa sahihi vya usafi.

Soma Zaidi
Kampeni Za Haki za Binadamu

KIJANA NA MAAMUZI

Lengo la mradi ni kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika michakato ya kufanya maamuzi katika ngazi za jamii na serikali za mitaa. Mradi unalenga kuhamasisha vijana kupitia majadiliano ya mtandaoni (online) na ana kwa ana (offline), kwa kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii, mijadala ya jamii, na vipindi vya redio za mitaa ili kukuza sauti zao na kuhimiza utawala shirikishi.

Soma Zaidi
Miradi Ya Utunzaji wa Mazingira

TANZANIA YA KIJANI

Mradi unalenga kuhifadhi na kurejesha Hifadhi ya Msitu ya Mtuli na Hinju kupitia mipango endelevu inayoongozwa na jamii. Mradi unashirikisha vikundi kumi (10) vya ufugaji nyuki ili kukuza uhifadhi wa mazingira wakati huo huo ukianzisha fursa mbadala za kipato kwa jamii za eneo hilo.

Soma Zaidi
Miradi Ya Utunzaji wa Mazingira

USAFISHAJI WA FUKWE

Kuanzia mwaka 2022 hadi sasa, TASA (Tanzania Safety Alliance) imekuwa ikitekeleza Kampeni ya Usafi wa Pwani katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara. Kampeni hii ni mpango wa kimazingira unaongozwa na vijana wenye lengo la kukuza usafi wa ukanda wa pwani, uhifadhi wa mazingira, na uwajibikaji wa jamii

Soma Zaidi
Miradi ya Haki Za binadam

BODABODA BALOZI WA AMANI

Kampeni ya Kuwawezesha Bodaboda Kuwa Mabalozi wa Ujenzi wa Amani, iliyotekelezwa kwa kushirikiana na GNRC (Global Network of Religions for Children) chini ya Mpango wa Vijana Katika Vitendo (Youth in Action Programme), inalenga kuwashirikisha waendesha pikipiki (bodaboda) kama wadau wakuu wa amani na mabadiliko chanya ndani ya jamii zao.

Soma Zaidi