• Nyumbani
  • Kuhusu
  • MiradiTazama miradi yetu
  • Habari na Blogu
  • Contact Us

Rasmi: Tanzania Safety Alliance (TASA) Imeanza Mfululizo wa Mafunzo ya Kuimarisha Uwezo wa Taasisi (OCD) Kupitia Programu ya Vijana Plus

Febuari 16, 2026

Tasa Tanzania

Uncategorized

Shirika la Tanzania Safety Alliance (TASA) limeanza rasmi mfululizo wa mafunzo ya kuimarisha uwezo wa kitaasisi (Organizational Capacity Development) kwa lengo la kuboresha mifumo ya utendaji na uendelevu wa shirika.

Mafunzo haya yanayowezeshwa na Save the Children kupitia programu ya Vijana Plus, ni sehemu ya mkakati endelevu wa kutoa miongozo ya kiufundi kwa washirika wa maendeleo. Katika siku ya kwanza ya mfululizo huu, timu ya TASA imejikita katika mada za Mpango Mkakati (Strategic Plan) na Mpango wa Mwaka (Annual Plan) ili kuoanisha dira ya shirika na utekelezaji wa afua za mradi.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa TASA inakuwa na mifumo madhubuti ya upangaji wa shughuli, usimamizi wa rasilimali, na upimaji wa matokeo ya muda mrefu. Kwa kuimarisha Mpango Mkakati, shirika linajiweka katika nafasi nzuri ya kutoa huduma zenye tija na zenye mwelekeo wa matokeo (Results-Based Management) kwa walengwa.

Iliyotangulia: TASA Yashiriki Warsha ya Ujenzi wa Amani na Haki za Binadamu Dar es Salaam
Inayofuata TASA Yaimarisha Uandishi wa Maandiko Miradi na Usimamizi wa Ruzuku, Ikiwa ni Sehemu ya Pili Ya Utekelezaji wa OCD chini ya Vijana Plus Project

Search

Archives

  • Machi 2026
  • Febuari 2026
  • Oktoba 2025

Categories

  • Uncategorized

About TASA

TASA is a Non Governmental Organization committed to fostering safety society, free from violence. Guided by its vision of a safe and inclusive environment, the Alliance promotes safety standards through public education, stakeholder engagement, and advocacy for policy and legal reforms.

Quick Links

  • Nyumbani
  • Kuhusu
  • MiradiTazama miradi yetu
  • Habari na Blogu
  • Contact Us

Contact Info

Physical Address: Mtwara-Tanzania Mtwara MC, chuno street (Map is attached in About Us Page)

Phone: +255786388501
E-mail: [email protected]
Website: https://tanzaniasafetyalliance.org

© Copyright 2026 Tanzania Safety Alliance. All Rights Reserved

Swahili
English